Mwanzoni, mtoto huyo wa mchungaji aliajiriwa kama mwalimu, kazi kubwa kwa mwafrika wakati huo, kwa sababu ajira bora na biashara lilikuwa eneo la wazungu pekee. Kaunda hakukubali mipaka hiyo, na aliingia katika siasa, hatua iliyomsababishia kufungwa jela mara kadhaa. Alimudu kuiongoza nchi yake kupata uhuru, na katika uchaguzi wa kwanza…